BancABC Prepaid Card ndio Kubwa Lao. Kadi salama yenye 3D

Kadi salama yenye ulinzi wa 3D ni nini?

3D ni Programu maalum iliyoundwa na VISA ili kumtambua mmiliki halali wa kadi kila anapofanya manunuzi mtandaoni. Huduma hii hufanya manunuzi mtandaoni yawe salama Zaidi kwa kukulinda dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa ya kadi yako ya BancABC. Hakuna haja ya kupakua programu yoyote au ya kujisajili ili kupata huduma hii.

Je Inafanyaje kazi?

Wakati unapofanya manunuzi yako ya kitu chochote mtandaoni iwe kwa kompyuta au kifaa chochote cha kidijitali, programu hii itakuelekeza kuhakiki taarifa zako kwa kukutumia ujumbe mfupi au barua pepe ikiwa na namba ya kuidhinishia muamala. Hii itasaidia kuthibitisha endapo muamala umefanywa na mmiliki halali wa kadi na kukulinda na wadukuzi/wezi wa mtandaoni.

Mtumiaji anafaidika vipi na programu hii?

Kupitia programu hii, mmiliki wa kadi ameongezewa ulinzi wa fedha zake kwani huzuia matumizi ya kadi yasiyoidhinishwa na mmiliki halali wakati wa kufanya manunuzi mtandaoni. Huduma hii inaiwezesha benki kutambua endapo muamala umefanywa na mmiliki halali wa kadi na kumlinda dhidi ya wizi wa mtandaoni ili hali ikimhakikishia mteja mambo yafuatayo:

  • Ulinzi wa fedha zake
  • Kujiamini wakati wa kufanya miamala mtandaoni
  • Amani ya moyo utambuapo kuwa fedha zako zipo salama
  • Huduma hii ni bure na rahisi kutumia

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara?

i. Je, taarifa zangu binafsi zipo salama?
Ndio, taarifa zako zipo sehemu salama na zimehifadhiwa kwa umakini wa hali ya juu.

ii. Je, Huduma hii ina gharama gani?
Hapana. Huduma hii ni bure.

iii. Je,  huduma hii ni maalumu kwa kadi za aina gani?
Huduma hii inapatikana kwenye aina zote za kadi za BancABC (Yaani prepaid na debit)

iv. Je, nitahitaji kupata kadi mpya au kadi nyingine ili kupata huduma hii?
Hapana. Kadi yako uliyonayo tayari imeunganishwa na huduma hii. Hauna haja ya kupata kadi nyingine.

v. Je, nitajuaje kama muamala wangu ninaoufanya mtandaoni una ulinzi wa 3D? Huduma hii hufanya kazi wakati wa malipo. Kumbuka, hautohitaji kupakua programu yoyote au kujisajili mahali popote ili kupata huduma hii. Pindi ufanyapo malipo mtandaoni, itafika mahali ambapo utaombwa namba ya kuidhinishia malipo ili kufanya utambuzi wako na yote hii ni katika kuhakikisha tunalinda fedha zako dhidi ya udanganyifu/wizi wa mtandaoni.

vi. Iwapo nitafikia hatua hii ya uthibitisho, ni kitu gani kitafuata?
BancABC itakutumia kwenye namba ya simu au barua pepe yako ambayo uliijaza kwenye fomu wakati wa kununua kadi, namba ya kuidhinishia muamala itakayotumika kwa awamu moja tu. Utakapofika kwenye hatua hii ya ziada, fuata maelekezo kwenye mtandao ili kukamilisha uthibitisho wako.


Je, nitaweza kutumia kadi yangu ya BancABC iwapo mtoa huduma mtandaoni hashiriki katika programu hii?
Ndio. Kadi yako ya BancABC itaendelea kufanya kazi kama kawaida hata kama mtoa huduma mtandaoni hashiriki kwenye kufanya uthibitisho huu. Miamala yako itaendelea kulindwa kwa ufanisi mkubwa na kuondoa kabisa  mianya ya kutokea kwa wizi mtandaoni .

 

PATA KADI YAKO SALAMA YENYE 3D

 
 

For secure, convenient fast and reliable 24 hour banking

Investor Relations

BancABC aims to provide the investor community with transparent and timeous information. This is undertaken through a proactive process whereby information is continually and broadly disseminated to the financial community and the investing public, ensuring that the Group is accurately valued in the marketplace...

Visit investors page